top of page

Rangi ya kinyesi na maana yake kitaalamu| ULY CLINIC

Updated: Mar 16, 2022


Kinyesi huweza kuwa na rangi aina tofautu tofauti, Aina hizo hutokana na chakula ulichokula au ugonjwa fulani ndani ya mwili kinyesi cha rangi ya kijani huchukuliwa kama rangi za kawaida.


Aina chache za rangi ya kinyesi hushukiwa kwamba kuna kitu Fulani mwilini hakiko sawa ama kuna ugonjwa ndani ya mwili unaotakiwa kutibiwa


Rangi ya kinyesi mara nyingi huathiriwa na nini unachokula na kiasi cha nyongo kilichotolewa na kibofu cha nyongo. Nyongo ni majimaji yenye rangi ya njano kuelekea kijani yanayotumika kumen’genya chakula chenye mafuta.


Nyongo inapokuwa inasafili kwenye utumbo hubadilishwa na vimengenya vingine na kubadilika rangi kutoka kijani kwenda Kahawia. Kinyesi cha binadamu hupewa rangi yake asiliana nyongo.


Kama kinyesi chako kina rangi nyekundu ambapo inamaanisha kuwepo kwa damu mtafute daktari wako kwa matibabu.


Aina tofauti ya rangi ya kinyesi na maana zake na nini kinachosababisha rangi hiyo


Rangi ya kijani


Inamaanisha nini?


Kuwa na rangi ya kijani inaweza kumaanisha kuwa chakula wakati kipo kwenye utumbo kilikuwa kinapita kwa kasi zaidi, mfano kwa sababu ya kuhara n.k. Kupita kwa kasi hiyo husababisha nyongo kutopata muda wa kumen’genya chakula hicho ipasavyo na hivyo kutoka kama kilivyo au pasipo kumengenywa vema na nyongo.


Chakula na dawa zinazoweza kusababisha kinyesi kuwa na rangi ya kijani ni nini?


Kula Mboga za kijani kwa wingi, vyakula vyenye rangi ya kijani kama vyakula/vinywaji vyenye rangi ya kijani na vidonge vya madini chuma huweza kupelekea kupata kinyesi cha kijani.


Rangi mpauko ama rangi ya udongo


Nini huweza kusababisha?


Kukosekana kwa nyongo katika kinyesi. Hii inaweza kumaanisha kuwa mirija inayopitisha nyongo imeziba. Mtu pia anaweza kuwa na dalili ingine ya manjano endapo mirija ya nyongo imeziba


Chakula au dawa zinazoweza kusababisha hali hii ni nini?


Aina Fulani za dawa, kama bismuth subsalicyclate na madawa mengine ya kuzuia kuhara husababisha mtu kuwa na kinyesi cha rangi hii.


Rangi ya njano na ya uterezi au inayonuka kama mnyama aliyekufa


Inamaanisha nini?


Kuwepo kwa mafuta mengi katika kinyesi, kama vile kwa sababu ya matatizo ya ufyonzaji wa chakula katika utumbo, kama ugonjwa wa celiac, na ugonjwa wa crohn's


Chakula kinachoweza kusaabisha ni nini?


Protini aina ya gluten inayopatikana kwenye chakula kama mkate na nafaka tofauti.


Mwone dakitari kwa vipimo zaidi endapo unapata choo hiki kwa muda mrefu


Rangi nyeusi


Inamaanisha nini?


Kuvia kwa damu katika sehemu za mwanzo za utumbo kama vile kwenye tumbo la chakula na utumbo mwembamba, hali hii ya kuvia huweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au majeraha ndani ya utumbo


Dawa ama vyakula vinavyoweza kusababisha hili ni nini?


Dawa za kuongeza damu zenye madini chuma, bismuth subsalicylate, ama matunda meusi kama furu, kula mkaa au udongo, juisi ya zabibu au juisi yenye rangi nyeusi, n.k huweza kusababisha choo kuwa cheusi. Hata hivyo kinyesi chenye nyongo nyingi huweza kuonekana kuwa kama cheusi kwenye mwanga hafifu, kikiangaliwa kwenye mwanga mwingi huonekana kuwa na rangi ya ya kijani inayoelekea nyeusi.


Rangi nyekundu


Humaanisha nini?


Kuvia kwa damu sehemu za mwisho za utumbo mdogo kama vile utumbo mpana na mkundu mara nyingi husabaishwa na bawasiri


Dawa/vyakula vinavyoweza kusababisha rangi hii ni kama


Vyakula vyenye rangi nyekundu, nyanya, ama juisi yake na vyakula vingine vyenye rangi nyekundu huweza kusababisha hali hi pia.


Kujua zaidi kuhusu rangi tofauti za kinyesi na maana zake kiafya bonyeza hapa


Tazama video hii kwa maelezo zaidi21,825 views1 comment

Recent Posts

See All

1 Comment
Like
bottom of page