top of page
Writer's pictureDr. Benjamin Lugonda, MD

Vihatarishi vya kupata saratani ya tumbo


Vyakula vya kubanika kwa moshi hukuweka hatarini kupata saratani ya tumbo

Nini husababisha saratani ya tumbo?


Madakitari hawana uhakika nini husababisha saratani ya tumbo. Kunauhsiano mkubwa sana kati ya chakula kilichookwa moshi, chenye chumvi nyingi sana au kilichohifadhiwa kwenye chumvi nyingi na saratani ya tumbo.

Saratani hii imeonekana kupungua Duniani na kwa kiasi kikubwa kwenye maeneo yenye matumizi makubwa ya friji-fridge kama njia ya kuhifadhia chakula badala ya njia zingine kama zilizotajwa hapo juu.


Kwa ujumla saratani huanza pale kunapokuwa na mabadiliko kwenye vinasaba au kitaalamu DNA na mabadiliko haya husababisha chembe hai kuzaliana pasipo kudhibitiwa au kuishi muda mrefu kulicho chembe nyingine na hivo mkusanyiko wa chembe hizi hutengeneza uvimbe na unaweza kuvamia kwa kugandamiza maeneo jirani.


Vipi ni vihatarishi vya kupata saratani ya tumbo-gastric cancer?


Vihatarishi vifuatavyo vimeonekana kuambatana na saratani ya tumbo

  • Chakula/mlo wenye chenye chumvi nyingi au kilichookwa kwa moshi

  • Mlo wenye matunda kidogo na mboga za majani

  • Kula chakula cha uyonga wenye sumu ya aflatoxin(kama karanga n.k)

  • Maambukizi ya bakiteria aitwaye helicobacter pyroli

  • Michomo ya muda mrefu tumboni(inflamation) kutokana na vidonda vya tumbo na magonjwa mengine

  • Maambukizi ya kirusi anayesababisha upungufu wa damu uitwao pernicious anemia

  • Uvutaji wa sigara

  • Maoteo ya vinyama kama vidole kwenye kuta za tumbo kitaalamu stomach polyps

Dalili za saratani ya tumbo ni zipi?


Dalili zinapotokea maranyingi humaanisha saratani imesambaa au imekuwa kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba matibabu yake huwa ni magumu. Ikiwa mtu anaonyesh adalili anaweza kuwa na kati ya hizi zifuatazo;

  • Kuchoka/uchovu

  • Kuhisi tumbo limejaa baada ya kula

  • Kushiba haraka baada ya kula chakula kidogo sana

  • Kiungulia ambacho ni kikali na kinachoendelea wakati wote

  • Kuhisi chakula hakijamengenywa(tumbo kujaa)

  • Kichefuchefu kinachoendelea na kisichoelezeka kimesababishwa na nini

  • Maumivu ya tumbo

  • Kutapika kusikoisha

  • Kupungua uzito bila sababu

Siku zote tafuta ushauri kwa wataalamu wa afya endapo una dalili ambazo huzielewi, Kupata msaada wa ki Afya unaweza tutafuta katika namba zetu hapo chini ili tukukutanishe na madaktari wabobezi wakuhudumie. Karibu sana

35 views0 comments

Recent Posts

See All

Σχόλια


bottom of page