top of page

SERA ZETU

Sera ya marekebisho ya habari

ULY CLINIC inajitahidi kutoa habari za afya za ukweli, zinazotokana na tafiti za kisayansi na utafiti wa kitaalamu. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila makala na habari inayochapishwa kwenye tovuti yetu ni ya uhakika, sahihi, na yenye manufaa kwa jamii. Ikiwa kuna habari yoyote inayochanganya, kupotosha au kuwa na taarifa zisizo sahihi, habari hiyo itarekebishwa mara moja au kuondolewa, ili kuhakikisha kuwa tunatoa tu habari za kweli na sahihi kwa watumiaji wetu.

Tafadhali kumbuka: Hakuna habari zilizorekebishwa kwa sasa.

Mwongozo wa kutoa link kwa tovuti ya ULY CLINIC kwenye kurasa za mtu binafsi

Ikiwa unataka kutumia tovuti ya ULY CLINIC kama chanzo cha habari za afya kwa lengo la kutoa elimu na si kwa madhumuni ya kibiashara, tafadhali fuata miongozo hii:

  1. Anza kwa kutumia neno "Chanzo: ULY CLINIC" ili kuthibitisha uhalali wa taarifa na kutoa heshima kwa haki za miliki.

  2. Tunga kiunganishi (link) kwenye sehemu husika ya makala au mada unayotaka jamii ielimike, kuhakikisha kuwa unaleta habari kwa usahihi na kutunza maadili ya kipekee ya tovuti yetu.

Sera ya kukopi na kutumia mada zetu

ULY CLINIC inaruhusu matumizi ya makala na mada zilizochapishwa kwenye tovuti yetu kwa madhumuni ya elimu tu. Hata hivyo, si kwa madhumuni ya biashara. Masharti yafuatayo lazima yazingatiwe:

  1. Hakuna matumizi ya kibiashara: Hairuhusiwi kutumia makala za ULY CLINIC kwa lengo la kujinufaisha kibiashara au kupotosha jamii.

  2. Kukopi na kutumia picha: Hairuhusiwi kukopi picha au makala na kutumia kwenye tovuti yako au kurasa za mitandao ya kijamii bila idhini ya maandishi kutoka kwa ULY CLINIC.

  3. Kujenga kiunganishi (link): Unaruhusiwa kutangaza makala zetu kwa kutumia kiunganishi kutoka kwa tovuti yetu na kutoongeza wala kupunguza chochote kwenye makala zilizochapishwa.

  4. Haki za Miliki: Makala yetu na picha ni mali ya ULY CLINIC, na kwa hiyo, zinapaswa kutumika kwa heshima na kwa mujibu wa sheria.

Matumizi yanayohusiana:
  • Kuchapisha makala: Unapochapisha makala za ULY CLINIC kwenye tovuti yako au kwenye vyombo vingine vya mtandao, hakikisha unahusisha kiunganishi cha tovuti yetu na uandike "Chanzo: ULY CLINIC".

  • Kufanya Re-publishing: Hairuhusiwi kuchapisha tena makala za ULY CLINIC bila kupata idhini ya maandishi kutoka kwa timu yetu. Hii ni kuhakikisha kwamba hakutokuwepo na uhalifu wa hati miliki.

Kwa nini sera hizi ni muhimu?

Sera hizi zipo ili kulinda haki za kiakili na kuhakikisha kuwa habari zinazotolewa kwa jamii zinakuwa za kweli, sahihi na zenye manufaa kwa afya ya watu. Tunawahimiza watumiaji wetu kutii masharti haya ili kuwa na ushirikiano wa kisheria na kuhakikisha kwamba kila mtu anafaidika na elimu ya afya inayoletwa na ULY CLINIC.

Nashukuru kwa kutufuatilia na kuzingatia sera hizi kwa usahihi, ili kuendeleza juhudi zetu za kutoa elimu ya afya bora kwa Kiswahili.

Imeboreshwa 12.04.2025

bottom of page