top of page
Soriasisi ya viganja vya mikono-ulyclini

Na ULY CLINIC

Soriasisi ya viganja vya mikono na kanyagio

Utangulizi

 

Soriasis ni ugonjwa sugu wa ngozi unaotokana na michomo endelevu  ya kinga za mwili za mtu. Ugonjwa husababisha mwonekano wa unaoeleweka wa maeneo wa wekundu, magamba(ngozi kuwa nene). Kuna aina kadhaa za tatizo hili zinafahamika, na huweza kuonekana kwenye vianja vya mikono tu, au mikono na miguu au mwili mzima

 

Ugonwja huu unahusianishwa na magonjwa mengine kama vile athraitis, ugonjwa wa crohn's, yuveitis na ugonjwa wa seliak

 

Dalili

 

 • Viganja au kanyagio huonekana kuwa na rangi nyekundu kabisa au kiasi

 • Ngozi kuwa kavu au nene

 • Mipasuko au mifereji ya mipasuko kwenye ngozi

 • Kutokwa damu kwenye mipasuko ya ngozi

 • Kucha kuwa nene na zenye mabonde

 • Kucha kuwa na vijishimo na kuingia ndani

 • Magamba ya ngozi kuwa magumu na enye ncha na yenye kufanana

 • Ugonjwa kuwepo kwa muda mrefu

 

Magonjwa mengine yanayofanana na dalili


Kumbuka ugonjwa huu unaweza kufana tabia na 

Kisababishi

 

Ni nini husababisha soriasisi?

Hakuna sababu inayoeleweka kupelekea kutokea kwa soriasis kwenye mikono hata hivyo sababu zifuatao zinaweza kuamsha tatizo hili kwenye mikono na hivyo hufahamika kama vihatarishi

 

 • Majeraha yoyote kwenye ngozi

 • Maambukizi kwenye ngozi

 • Matatizo mengine ya ngozi kama Demaraitizi ya mikono

 • Kuwa na msongo wa mawazo

 • Matumizi ya aina fulani ya dawa kama dawa jamiiya lithium 

 • VIhatarishi

 • Uzito mkubwa(ugonjwa wa obeziti)

 • Unywaji wa pombe kupita kiasi

 • Kuvuta sigara au tumbaku

 • Kuwa na historia kwenye familia ya tatizo hili

 


Jinsi tatizo linavyotambuliwa


Tatizo hutambuliwa kwa mwonekano wake tu wa nje na daktari, tatizo hweuza kuonekana sehemu nyingine ya mwili kama sehemu a dalili ya soriasi, ili kutofautisha tatizo hili na matatizo mengine kama tinea pedis, kipimo cha bayopsi cha kuangalia maghamba kwenye ngozi kinapaswa kufanyika

Matibabu

Matibabu yasiyo dawa

 • Kupunguza uzito

 • Kufanya mazoezi yenye mpangilio maalumu

 • Kudhibiti msongo wa mawazo

 • Kuacha kuvuta sigara

 • Kutibiwa matatizo mengine ya kiafya

Matibabu dawa

 • Mafuta ya kulainisha ngozi- tumia mafuta mazito kama vasselin blue seal,au mafuta ya krimu, paka mara kwa mara kuzuia ngozi isikauke na pia yanayweza kusaidia kupunguza maumivu ya mpasuko wa ngozi

 • Dawa za kuondoa magamba- mchanganyiko wa dawa zenye kiini cha urea. salicyclic asid

 • Matumizi ya uji mzito wa rami- paka kwenye maeneo yaliyoathirika haswa wakati wa usiku- huondoa magamba na kupunguza michomo ya kinga za mwili

 • Dawa jamii ya steroid- hupunguza miwasho, na michomo ya kinga za mwili na magamba. Kwa matumizi ya dawa hii kutibu tatizo lako muulizedaktari wako

Dawa kwa tatizo sugu

Wasiliana na daktari wako kama una tatizo sugu la soriasis. Hata hivyo daktari anaweza kutumia dawa zifuatazo kwa tatizo sugu la soriasis;

 • PUVA

 • Acitretin

 • Methotrexate

Imeboreshwa mara ya mwisho, 31.10.2020

ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kaifya

 

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na tiba kupitia namba za simu au kubonyeza pata tiba chini ya tovuti hii.

Bonyeza hapa kurejea kwenye mada zingine za ngozi

Rejea za mada hii,

bottom of page