top of page

Tezi za binadamu

Sehemu hii utajifunza kuhusu tezi mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu ikiwa ni tezi za endokrain na zisizo za endokrain.

Pineal

Pineal

Pineal Hii tezi iliyopo sehemu ya ndani ya ubongo. Jina lake limetokana na umbo la tezi hiyo kufanana na pinecone. Tezi hii huzalisha homoni ya melatonin.

Adreno

Adreno

Tezi za adreno ni jozi ya tezi mbili zilizopo juu ya kila figo. Tezi hizi zina umbo la piramidi. Kwa mtu mzima tezi moja inaweza kuwa na urefu wa sentimita 3 hadi 5, upana wa sentimita 2 hadi 3 na unene wa sentimita 1, huku uzito wa tezi moja unaweza kuwa gramu 3.5 hadi 5.

Parathairoidi

Parathairoidi

Tezi za parathairoidi ni tezi nne ndogo zilizopo nyuma ya tezi ya thairoidi inayopatikana mbele ya koromeo maeneo ya shingo.Kati ya tezi hizi nne, mbili zipo kulia na mbili kushoto ya tezi ya thairoidi, nyuma ya kila bawa la tezi ya thairoidi.

Haipothalamasi

Haipothalamasi

Haipothalamas (hypothalamus) ni sehemu ndogo ya ubongo yenye kazi muhimu katika mfumo ya fahamu na homoni.

bottom of page