Imeandikwa na ULY CLINIC
Tiba shufaa- palliative care
Tiba shufaa ni tiba inayotolewa mahususi kwa watu wenye magonjwa sugu ambao wameumwa kwa muda mrefu bila kupata uponyaji. Tiba hii licha ya kuwa imeanza miaka mingi iliyopita imekuwa maarufu kwenye jamii kwa sasa kutokana na kuongezeka kwa visa vya saratani. Hata hivyo tiba hii si mahususi tu kwa wagonjwa wa saratani bali malengo yake ni kutolewa kwa wagonjwa wote wenye magonjwa au matatizo ya kimwili yaliyo endelevu na yasiyotibika.
​
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO huduma za tiba shufaa ni aina ya matibabu inayoboresha ubora wa maisha ya mgonjwa na familia iliyo katika matatizo yatokanayo na kuuguliwa, kwa kuzuia na kupunguza matatizo katika maana ya kutambua mapema dalili za tatizo na namna ya kuhakiki tatizo na kutuliza maumivu na matatizo mengine ya kimwili, kijamii, kiakili na kiroho kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu.
​
Mbali na kupunguza maumivu na kuongeza ubora wa maisha, tiba shufa hulenga kusaidia wagonjwa kuelewa na kufanya uchaguzi wa tiba wanazotarajia kupokea.
​
​
Magonjwa yanayohitaji tiba shufaa ni mengi kama vile;
​
-
Magonjwa sugu katika hatua za mwisho
-
Ajali za ghafla
-
Kuzaliwa na uzito mdogo sana kupita kiasi
-
Madhaifu ya uzeeni
-
Kufeli kwa moyo
-
COPD
-
Ugonjwa wa Parkinson's
-
Saratani
-
N.k
Kina nani wanahusika kutoa tiba shufaa?
​
Kwa kawaida, tiba shufaa hutolewa kutuliza maumivu na matatizo mengine ya kimwili, kijamii, kiakili na kiroho kwa wagonjwa wenye magonjwa sugu. Kwa mantiki ya maana hii tiba shufaa huhusisha watu watu wenye taaluma hizi
-
Daktari
-
Nesi
-
Mhudumu wa afya ya jamii
-
Mtaalamu wa saikolojia na magonjwa ya akili
-
Mtaalamu wa lishe
-
Mchungaji au Shehe
-
Na wengine kutokana na mahitaji ya mgonjwa
Tiba gani zingine zinafanana na tiba shufaa?
Tiba shufaa hutaka kufanana na tiba hospice ambayo hutolewa ikifanana na tiba shufaa nyumbani au hospitali. Tiba shufaa hutofautiana na tiba hospice kwa sababu, katika tiba hospice mgonjwa kwa hiari yake mwenyewe huchagua kutofanyiwa matibabu yanayolega uponyaji au ya kurejesha nyuma tatizo hali akijua kwamba tatizo halitibiki na hana muda mrefu wa kuishi. Tiba hii licha ya kuwa tofauti na tiba shufaa bado hutumia mbinu za tiba shufaa katika kumfariji mgonjwa na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Tiba hii mara nyingi huchaguliwa na mgonjwa ambaye alishataarifiwa na daktari kwamba endapo hatapokea matibabu anaweza ishi chini ya miezi sita ijayo.
Kanuni za tiba shufaa
-
Huthibitisha uhai na kuchukulia kifo kama mchakato wa kawaida katika maisha
-
Haizuii wala kuharakisha maisha
-
Hupunguza maumivu na dalili zingine za kufadhaisha
-
Huunganisha tiba ya saikolojia na kiroho katika matibabu
-
Inatoa mfumo wa msaada kusaidia wagonjwa kuishi kikamilifu iwezekanavyo hadi kifo
Sehemu gani unaweza kupata huduma za tiba shufaa?
​
Huduma za tiba shufaa hutolewa mahari mgonjwa na ndugu wanapopendelea mkuzipokea kwa jinsi inavyowezekana. Huduma hizi si kwamba zinatolewa hospitali tu unaweza zipata sehemu hizi zifuatazo;
-
Nyumbani
-
Hospitali
-
Hospice
-
Kwenye maeneo maalumu ya hkutunza wazee
​
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa maelezo zaiid na ushauri kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii.
​
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu zaidi na ushauri kupitia namba za simu au kubonyeza pata tiba chini ya tovuti hii.
Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu mada mbalimbalii za kiafya
​
Imeboreshwa, 30.11.2020
​
-
WHO. Palliative care. https://www.who.int/health-topics/palliative-care. Imechukuliwa 28.11.2020
-
Web MD. Palliative care. https://www.webmd.com/palliative-care/what-is-palliative-care#2. Imechukuliwa 28.11.2020
-
NIA. What Are Palliative Care and Hospice Care?. https://www.nia.nih.gov/health/what-are-palliative-care-and-hospice-care. Imechukuliwa 28.11.2020
-
Mediline plus. What is palliative care?. https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000536.htm. Imechukuliwa 28.11.2020
-
What Is Palliative Care? The Principles That You Need To Know. https://hellocaremail.com.au/principles-palliative-care-need-know/. Imechukuliwa 28.11.2020