Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Tumbo kuuma
​
Tumbo kuuma au maumivu ya tumbo ni dalili inayofahamika sana, mara nyingi husababishwa na matatizo ya mvurugiko wa tumbo na utumbo hivyo si hali ya kuogopesha mara zote kama maumivu si makali.
Maumivu ya ghafla na yaliyo makali sana ni dalili ya kuogopesha na humaanisha kuna ugonjwa ndani ya tumbo ambayo ni magonjwa ya michomo tumboni na magonjwa ya upasuaji yanayohitaji matibabu ya dharura.
Magonjwa ya upasuaji yanayohitaji matibabu ya upasuaji wa dharura ni kama vile, michomo ya kidole tumbo (apendisaitis), kuziba kwa utumbo, kutoboka kwa tumbo kutokana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo au daivetikulaitis, mimba ya ekitopiki (mimba kutungwa nje ya mfuko wa kizazi au mimba) iliyotungwa nje ya mfuko wa kizazi kupasuka, kujinyonga kwa sisti ya ovari, anyurizimu kuvilisha damu tumboni, embolizimu ya mezenteriki, thrombosis, magonjwa ya njia ya biliari, pankreataitis, na mawe kwenye figo.
Gangrini ya utumbo na kutoboka kwa utumbo kunaweza kutokea chini ya masaa sita baada ya kuziba kwa mishipa ya damu ya tumbo kutokana na apendisaitis, kujinyonga kwa utumbo au jiwe la embolaz kwenye mishipa ya damu ya arteri.
​
Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu mada hii
​
Muulize daktari wako siku zote endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba kabla ya kufanya maamuzi yoyote.
​