Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Azuma inatibu UTI?
Kama unamaanisha Azuma yenye azithromycin, kwa kawaida si antibayotiki inayopendekezwa kutibu UTI ya kawaida. Azithromycin hutumika zaidi kwa baadhi ya maambukizi ya njia ya hewa, ngozi na baadhi ya maambukizi ya zinaa.
Kwa UTI, antibiotic huchaguliwa kulingana na aina ya UTI, bakteria anayesababisha maambukizi na usugu wa dawa. Miongozo ya sasa ya UTI haitaji azithromycin kama chaguo la kawaida la kutibu UTI.
Kwa hiyo, usitumie Azuma kwa kudhani tu kwamba ni dawa ya UTI. Kama una dalili kama kuwaka wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, maumivu chini ya tumbo, homa au maumivu ya kiuno, ni vizuri kupimwa mkojo na kupata antibayotiki inayolingana na hali hiyo.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
13 Septemba 2026, 15:06:30

