top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 12:26:22

Je dawa ya malaria ya Alu inatembe ngapi na natumia kwa siku ngapi naona daktari kaniandikia nikachukue

ALU 20 mg/120 mg kwa mtu mzima mwenye kilo 35 au zaidi:


Siku ya 1:

  • Vidonge 4 mara ya kwanza
  • Vidonge 4 tena baada ya saa 8

Siku ya 2:

  • Vidonge 4 asubuhi
  • Vidonge 4 jioni

Siku ya 3:

  • Vidonge 4 asubuhi
  • Vidonge 4 jioni

Jumla: vidonge 24 kwa siku 3.


ALU inapaswa kutumika pamoja na chakula au kinywaji chenye mafuta, kwa mfano maziwa, kwa sababu chakula chenye mafuta husaidia mwili kufyonza lumefantrine vizuri.


Kumbuka Fuata maelekezo ya daktari wako kuhusu umezaji wa dawa kwa kuwa haya ni maelezo ya kielimu tu na sio mbadala wa ushauri wa daktari.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

2 Septemba 2026, 08:20:14

​

bottom of page