top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 17:18:13

Je kama mwanamke anazingatia dawa vizuri kwa wakati anaweza kuambukiza VVU kwa yale maji maji ya ukeni?

Ikiwa mwanamke mwenye VVU anatumia dawa za ARV vizuri na kwa wakati, lakini jambo muhimu zaidi ni kama viral load yake imefikia kiwango kisichoonekana (Kisichotambulika).


  • Ikiwa anatumia ARV vizuri na nakala za virusi hazitambuiki na imeendelea kubaki hivyo, hawezi kuambukiza VVU kwa mwenzi wake kupitia ngono, hata kama majimaji ya uke yanagusa sehemu za siri. Hii huitwa K=K (Kisichotambulika = Kisichoambukiza).
  • Kuwa anatumia dawa tu hakutoshi kuthibitisha K=K; kipimo cha viral load ndicho kinachoonyesha kama virusi vimedhibitiwa kikamilifu.
  • Ikiwa nakala za virusi bado zinaonekana (Kutambulika), bado kuna uwezekano wa kuambukiza kupitia majimaji ya uke wakati wa ngono.

Kwa hiyo, ARV → viral load kushuka → ikiwa inakuwa na kubaki undetectable → hakuna maambukizi ya VVU kupitia ngono (K=K).


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

31 Agosti 2026, 13:10:36

​

bottom of page