top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Je maziwa kuuma baada ya kutumia dawa za kutoa mimba ya mwezi ni huashiria nini?

Maumivu ya matiti/chuchu baada ya kutumia dawa za kutoa mimba ya ujauzito wa mwezi yanaweza kutokea kwa sababu viwango vya homoni za ujauzito havishuki mara moja baada ya ujauzito kutoka.


Kwa hiyo, maumivu ya matiti yanaweza kuendelea kwa siku kadhaa hadi wiki chache na si lazima yawe ishara kwamba utoaji mimba haukufanikiwa.


Hata hivyo:

  • Kama maumivu yanaendelea bila kupungua, au bado una dalili nyingine za ujauzito, ni vizuri kufanya kipimo cha ujauzito baada ya muda unaofaa ili kuthibitisha kuwa ujauzito umeisha.
  • Kama ulitumia dawa lakini hukutokwa damu kabisa, au una maumivu makali ya tumbo, damu nyingi sana, homa, kizunguzungu/kuzimia au uchafu wenye harufu mbaya, nenda hospitali kwa uchunguzi.
  • Usitumie dawa nyingine za kutoa mimba bila ushauri wa mtaalamu.

Kwa kifupi: maumivu ya matiti pekee baada ya kutoa mimba kwa dawa yanaweza kuwa kutokana na mabadiliko ya homoni na hayathibitishi kwamba ujauzito bado upo.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

5 Septemba 2026, 14:50:47

​

bottom of page