top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

30 Septemba 2026, 09:07:17

Je mba zinatibika?

mba inaweza kutibika, lakini tiba hutegemea chanzo. Magamba na muwasho wa kichwa vinaweza kusababishwa na:


  • Fangasi wa kichwani (Tinea Kapitisi) – huweza kusababisha magamba, kuwasha na nywele kukatika.
  • Demataitisi ya Seboreiki – husababisha magamba na kuwasha, wakati mwingine magamba huwa na mafuta.
  • Soriasis ya kichwani – husababisha magamba mazito, makavu na kuwasha.
  • Dandrafu – mba ya kawaida inayosababisha magamba na kuwasha.
  • Demataitisi ya mguso – muwasho au mzio kutokana na shampoo, mafuta au bidhaa za nywele.
  • Maambukizi kwenye mashina ya nywele – kuvimba kwa vinyweleo, kunaweza kusababisha vipele na ukoko.

Kama ni fangasi kichwani, mara nyingi huhitaji dawa za fangasi za kunywa kama terbinafine au griseofulvin; shampoo ya ketoconazole au selenium sulfide inaweza kusaidia lakini kwa kawaida haitoshi pekee yake. Ni muhimu kutambua chanzo kwa sababu hali hizi hutibiwa tofauti.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

7 Septemba 2026, 20:15:00

​

bottom of page