Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 10:50:40
Je mwanamke akikunyonya uume kuna uwezekano wa mwanaume kupata magonjwa?
Mwanaume anaweza kupata baadhi ya maambukizi ya zinaa ikiwa mwanamke anamnyonya uume, ingawa hatari hutofautiana kulingana na maambukizi na hali ya mdomo wa mwenza.
Maambukizi yanayoweza kuambukizwa kupitia ngono ya mdomo ni pamoja na:
- Gonorea (kisonono) — inaweza kuambukizwa kutoka kooni kwenda kwenye uume na kusababisha uchafu au kuungua wakati wa kukojoa.
- Klamidia — inaweza kuambukizwa, ingawa si kwa ufanisi mkubwa kama gonorea.
- Herpes (HSV) — hasa ikiwa kuna vidonda vya herpes mdomoni.
- Kaswende — inaweza kuambukizwa ikiwa kuna kidonda cha kaswende mdomoni au kwenye sehemu za siri.
- HPV — inaweza kuambukizwa kupitia mgusano wa ngozi wakati wa ngono ya mdomo.
- HIV — hatari kupitia ngono ya mdomo ni ndogo sana, lakini si sawa na kutokuwepo kabisa; hatari huongezeka ikiwa kuna damu, vidonda mdomoni au kwenye uume, au maambukizi mengine ya zinaa.
Maambukizi mengine ambayo ni nadra ni kama;
- Maambukizi ya fangasi (Kandida): yanaweza kuathiri uume, hasa ikiwa kuna mazingira yanayorahisisha ukuaji wa fangasi.
- Maambukizi ya bakteria wa mdomoni: bakteria wa kawaida wa kinywa wanaweza kuingia kwenye michubuko au majeraha kwenye uume na wakati mwingine kusababisha maambukizi.
Kondomu wakati wa ngono ya mdomo hupunguza hatari ya maambukizi haya.
Ikiwa baada ya ngono ya mdomo kuna uchafu wa njano kwenye uume, kuungua wakati wa kukojoa, vidonda, malengelenge au uvimbe, ni muhimu kupima magonjwa ya zinaa kama gonorea na klamidia badala ya kusubiri dalili ziishe zenyewe.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
2 Septemba 2026, 18:24:41

