Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
27 Septemba 2026, 15:07:11
Je ni kipimo gani cha UKIMWI kinasubili miezi 3 au wiki 12?
Kipimo kinachoweza kusubiri hadi wiki 12 (siku 90) ni hasa kipimo cha maambukizi ya VVU kinachotafuta kingamwili pekee (Kipimo cha antibodi).
Hiki ndicho kinachotumika kwenye vipimo vingi vya haraka vya maambukizi ya VVU, ikiwemo baadhi ya vipimo vya kidoleni. Kipimo cha antibody kinaweza kugundua VVU kwa kawaida ndani ya siku 23–90 baada ya maambukizi. Kwa hiyo, kwa kipimo hiki, siku 90 (wiki 12/miezi 3) hutumika kama mwisho wa kipindi cha kusubiri.
Kwa ufupi:
- Kipimo cha haraka cha Antibodi tu: siku 23–90 → wiki 12 ni mwisho wa window period.
- Kipimo cha haraka cha antijeni/antibodi ya kidoleni: siku 18–90.
- Ag/Ab ya maabara kwa damu ya mshipa: siku 18–45.
- NAT/RNA: siku 10–33.
Kwa hiyo, ikiwa kipimo ni Vipimo vya haraka vya VVU, na kimefanyika siku 90 baada ya tukio la mwisho la hatari, kikawa negative na hakukuwa na tukio jipya la hatari katika kipindi hicho, matokeo hayo yanachukuliwa kuwa ya kuaminika kwa tukio hilo.
Muhimu: kama kulikuwa na matumizi ya PEP au PrEP, muda wa kutafsiri matokeo unaweza kuwa tofauti kwa sababu dawa za ARV zinaweza kuchelewesha kugundulika kwa maambukizi VVU.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
23 Agosti 2026, 23:47:19

