top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Je ni sahihi kuchelewa kupata hedhi kwa mama aliyejifungua zaidi ya mwaka na nusu?

Kuchelewa kupata hedhi baada ya kujifungua kunaweza kuwa kawaida, hasa kama mama bado ananyonyesha. Kunyonyesha huongeza homoni ya prolaktini, ambayo inaweza kuzuia ovulation na kuchelewesha kurudi kwa hedhi. Kwa baadhi ya wanawake, hedhi inaweza kuchelewa hadi wanapopunguza au kuacha kunyonyesha.


Lakini kama mtoto ana zaidi ya mwaka mmoja na nusu (miezi 18), si vizuri kudhani kuchelewa kwa hedhi kunasababishwa na kunyonyesha pekee. Mama anaweza pia kupata ujauzito kabla hata hedhi ya kwanza haijarudi, kwa sababu ovulesheni hutokea kabla ya hedhi.


Cha kufanya:

  • Kama amefanya tendo bila kinga, afanye kipimo cha ujauzito kwanza.
  • Kama kipimo ni hasi lakini hajapata hedhi kwa miezi 3 au zaidi, ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi. Sababu nyingine zinaweza kuwa mabadiliko ya homoni, sindromu ya ovari yeney vifukomaji vingi(PCOS), matatizo ya tezi ya thairoidi, msongo wa mawazo, kupungua sana uzito au baadhi ya dawa.
  • Kama bado ananyonyesha mara kwa mara, hasa usiku, kunyonyesha kunaweza kuwa sababu ya kuchelewa kwa hedhi, lakini kunyonyesha pekee si kinga ya kuaminika dhidi ya ujauzito baada ya miezi 6.

Kwa hiyo, baada ya miezi 18 bila hedhi, jambo la kwanza kuondoa ni ujauzito, kisha kutafuta sababu nyingine ikiwa bado hedhi haijarudi.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

5 Septemba 2026, 11:28:02

​

bottom of page