Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Je ovulesheni ya mtu akitoka kwenye hedhi ni siku ngapi?
Ovulesheni haiji siku maalum baada ya hedhi kwa kila mwanamke. Inategemea urefu wa mzunguko wa hedhi.
Kwa kawaida, ovulesheni hutokea takribani siku 14 kabla ya hedhi inayofuata.
Kwa mfano:
- Mzunguko wa siku 28 → ovulesheni karibu siku ya 14
- Mzunguko wa siku 30 → ovulesheni karibu siku ya 16
- Mzunguko wa siku 32 → ovulesheni karibu siku ya 18
- Mzunguko wa siku 24 → ovulesheni karibu siku ya 10
Kwa hiyo, si sahihi kusema kila mwanamke huanza ovulation siku fulani baada ya kumaliza hedhi. Kwa baadhi ya wanawake inaweza kutokea siku chache tu baada ya hedhi kuisha, hasa kama mzunguko ni mfupi.
Muhimu: Siku za kupata mimba huanza kabla ya ovulesheni, kwa sababu mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani ya njia ya uzazi kwa siku kadhaa.
Tumia kikokotoo cha ovulesheni kukokotoa tarehe ya ovulesheni kwa kubofya 👉Kikikotoo cha siku za hatari.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
3 Septemba 2026, 20:17:43

