top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 17:49:38

Je Ute mwingi katika kizazi huashiria nini?

Ute mwingi ukeni/kizazini unaweza kuwa wa kawaida au kuashiria tatizo, kulingana na aina ya ute na dalili zinazoambatana nao.


  • Ute wa kawaida: unaweza kuongezeka wakati wa siku za karibu na ovulesheni. Mara nyingi huwa mweupe au wa uwazi, hauna harufu kali, na hausababishi muwasho wala maumivu.
  • Ute mweupe mzito kama maziwa yaliyoganda, pamoja na muwasho au kuwaka, unaweza kuashiria fangasi (Kandida).
  • Ute wenye harufu kali ya samaki, hasa ukiwa mwembamba/kijivu, unaweza kuashiria Vajinosisiya bakeria (BV).
  • Ute wa njano/kijani, hasa ukiambatana na harufu, maumivu wakati wa kukojoa au maumivu wakati wa tendo, unaweza kuhusishwa na maambukizi ya zinaa, ikiwemo trikomoniasisi au maambukizi ya mlango wa kizazi.
  • Ute mwingi wakati wa ujauzito pia unaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya homoni, lakini ute wenye harufu mbaya, rangi isiyo ya kawaida, damu, maumivu au kuwasha unahitaji uchunguzi.

Kwa hiyo, wingi wa ute pekee hauwezi kutumika kutambua ugonjwa. Rangi, harufu, muonekano na dalili zinazoambatana nao ndiyo husaidia zaidi kujua chanzo.


Ikiwa ute ni mwingi lakini hauna harufu mbaya, hauna muwasho wala maumivu na ni wa uwazi/upe, mara nyingi unaweza kuwa ute wa kawaida wa uke.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

27 Agosti 2026, 09:03:14

​

bottom of page