top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 12:54:26

Kipimo cha sikoseli kinaweza kukosea wakati mwengine?

Ingawa vipimo vya kisasa ni vya kuaminika sana, kuna mazingira ambayo matokeo yanaweza kuathiriwa.


Mambo yanayoweza kusababisha tatizo ni pamoja na:


  • Kuongezewa damu hivi karibuni – damu ya mtu mwingine inaweza kuathiri matokeo ya kipimo.
  • Mtoto mchanga – aina na kiwango cha hemoglobini hubadilika kadiri mtoto anavyokua, hivyo baadhi ya majibu huhitaji kuthibitishwa baadaye.
  • Aina ya kipimo kilichotumika – baadhi ya vipimo ni vya screening tu na si vya kuthibitisha ugonjwa.
  • Magonjwa mengine ya hemoglobini, kama thalassemia au aina nyingine za hemoglobini, yanaweza kufanya tafsiri ya matokeo iwe ngumu.

Kwa hiyo, ikiwa majibu yamesema "chanya", "kubeba vinasaba vya seli mundu", "SS", au majibu hayalingani na historia ya mtu, si vizuri kuhitimisha bila kujua aina ya kipimo kilichofanyika.


Kipimo cha kuthibitisha, kama hemoglobin elekroforesisi au HPLC, kinaweza kutofautisha kwa usahihi zaidi kati ya ugonjwa wa seli mundu (mfano HbSS) na kuwa carrier/trait (HbAS).


Ikiwa kuna majibu mawili yanayopingana kwa mfano kipimo kimoja kinasema hana na kingine kinasema anayo majibu hayo yanafaa kuchunguzwa kwa kipimo cha kuthibitisha katika maabara.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

1 Septemba 2026, 14:12:38

​

bottom of page