Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 17:06:31
Kukokwa na damu mfululizo ukeni kunazuilika?
Ndiyo, kutokwa na damu mfululizo kunaweza kudhibitiwa, lakini matibabu hutegemea chanzo cha damu.
Sababu zinaweza kuwa:
- Mabadiliko ya homoni au matumizi ya uzazi wa mpango.
- Ujauzito au matatizo yanayohusiana na ujauzito.
- Maambukizi ya uke/kizazi au magonjwa ya zinaa.
- Faibroidi, polipsi au matatizo mengine ya kizazi.
- Matatizo ya tezi ya thairoidi au mfumo wa kuganda kwa damu.
- Baada ya kutoa mimba au kujifungua, damu inaweza kuendelea kwa kipindi fulani, lakini kutokwa damu kwa muda mrefu kunahitaji uchunguzi.
Usitumie dawa za kukata damu bila kujua chanzo. Daktari anaweza kuhitaji kufanya kipimo cha ujauzito, CBC/kipimo cha damu, uchunguzi wa uke na kizazi, au ultrasound kulingana na hali.
Ikiwa damu ni nyingi sana, kuna kizunguzungu/kuzimia, udhaifu mkubwa, maumivu makali ya tumbo, homa, au pedi kubwa inalowa ndani ya saa moja na hali inaendelea, nenda hospitali haraka.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
30 Agosti 2026, 12:13:05

