Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
27 Septemba 2026, 15:36:34
Kupanda boda(pikipiki) kila siku inaweza kua sababu mimba kutoka?
Kwa kawaida, kupanda boda/pikipiki hakusababishi mimba kutoka moja kwa moja, hata kama ni sehemu ya usafiri wa kila siku.
Mitetemeko ya pikipiki au barabara yenye mashimo kwa kawaida haiwezi kusababisha mimba kutoka. Mimba inalindwa ndani ya mfuko wa uzazi.
Hata hivyo, kuna hatari nyingine muhimu wakati wa kupanda pikipiki, hasa ajali, kuanguka au kugongwa, ambazo zinaweza kusababisha majeraha na wakati mwingine kuathiri ujauzito.
Kwa hiyo, ikiwa kuna uwezekano wa kutumia usafiri mwingine ulio salama zaidi, ni vizuri kuutumia, hasa kwenye barabara mbaya au safari ndefu.
Ikiwa baada ya kupanda pikipiki kuna kutokwa damu, maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo, maji kutoka ukeni, kizunguzungu au kuzimia, uchunguzi wa hospitali unahitajika.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
23 Agosti 2026, 11:21:04

