Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Kutokuona hedhi yako na umepima ukaona huna mimba hii inasababishwa na nini?
Kama kipimo cha ujauzito ni hasi, kuchelewa au kukosa hedhi kunaweza kusababishwa na:
- Mabadiliko ya homoni: hasa kuvurugika kwa homoni zinazodhibiti ovulesheni.
- Sindromu ya ovari yenye vifuko maji vingi (PCOS): inaweza kufanya hedhi iwe chache, ichelewe au ikosekane kabisa.
- Msongo wa mawazo, usingizi usio wa kutosha au mabadiliko makubwa ya uzito: vinaweza kuchelewesha ovulesheni na hivyo hedhi kuchelewa.
- Mazoezi makali au kula chakula kidogo sana: vinaweza kuvuruga mzunguko wa hedhi.
- Matatizo ya tezi thairoidi: yanaweza kusababisha hedhi kutokuwa ya kawaida.
- Kunyonyesha: homoni ya prolaktini inaweza kuzuia au kuchelewesha ovulesheni.
- Uzazi wa mpango wa homoni: kama njiti, sindano, vidonge au baadhi ya njia nyingine zinaweza kufanya hedhi ipungue au ikosekane.
Kama ulifanya ngono bila kinga hivi karibuni, kipimo kinaweza kuwa kimefanywa mapema. Rudia kipimo baada ya siku chache au pima angalau siku 21 baada ya tendo la mwisho lisilo na kinga.
Kama umekosa hedhi kwa miezi mitatu au zaidi bila kuwa mjamzito, ni vizuri kuonana na mtoa huduma wa afya ili kuchunguza homoni, Sindromu ya ovari yenye vifukomaji vingi (PCOS), thyroid na sababu nyingine.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
9 Septemba 2026, 13:18:26

