top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

27 Septemba 2026, 15:19:32

Kwani kipimo cha haraka cha kizazi cha 3 kinakua na uhakika mkubwa baada ya siku ngapi?

Kipimo cha haraka cha VVU cha kizazi cha 3 hutafuta kingamwili za VVU.


  • Wiki 4–6: Kinaweza kugundua maambukizi mengi, lakini negative bado haiwezi kuondoa VVU kabisa.
  • Wiki 8: Watu wengi huwa tayari wameunda kingamwili zinazoweza kugunduliwa.
  • Siku 90 (wiki 12): Huu ndio mwisho wa kipindi cha dirisha la matazamio kinachotumika kwa vipimo vya antibodi tu.

Kwa hiyo, ikiwa kipimo cha kizazi cha 3 kimefanyika siku 90 baada ya tukio la mwisho la hatari, na matokeo ni HASI, bila kuwa na tukio jipya la hatari katika kipindi hicho, matokeo hayo yanaaminika sana kwa tukio hilo.


Muhimu: Ikiwa kulikuwa na matumizi ya PEP au PrEP, muda wa kutafsiri kipimo unaweza kuwa tofauti.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

23 Agosti 2026, 23:41:26

​

bottom of page