top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Mimba inaweza kubaki bila kupata shida yoyote baada ya kuitoa, halafu ikatoka nusu?

Mimba inaweza kutoka kwa sehemu tu na baadhi ya tishu za ujauzito kubaki ndani ya kizazi. Hali hii huitwa mimba isivyokamilika kutoka au kuharibika . Miongozo inaeleza kuwa inaweza kutokea baada ya mimba kutoka yenyewe au baada ya kutoa mimba kwa dawa au njia nyingine.


Si lazima mtu awe na dalili kali mara moja. Hata hivyo, dalili zinazoweza kuonekana ni:

  • Kutokwa damu kwa muda mrefu au nyingi.
  • Maumivu au mikazo ya chini ya tumbo.
  • Kutoka mabonge au vipande vya tishu, huku baadhi ya tishu zikibaki ndani.

Muhimu: Kutokuwepo kwa maumivu au damu nyingi hakuthibitishi kwamba kila kitu kimetoka. Uchunguzi wa daktari, na wakati mwingine ultrasound, unaweza kuhitajika kuthibitisha kama kuna tishu za ujauzito zilizobaki.


Kama tishu zimebaki, kuna matibabu salama kulingana na hali ya mtu, kama kusubiri chini ya uangalizi, dawa au kuondoa tishu kwa njia ya kitabibu.


Nenda hospitali haraka ikiwa kuna damu nyingi sana, maumivu makali au yanayoongezeka, homa, harufu mbaya ukeni, kizunguzungu/kuzimia au udhaifu mkubwa, kwa sababu tishu zilizobaki zinaweza kuhusishwa na kutokwa damu au maambukizi.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

9 Septemba 2026, 17:25:36

​

bottom of page