Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
29 Septemba 2026, 15:29:50

Mimi nahisi joto usiku na mchana hata nikiwa kwenye feni nini shida?
Kuhisi joto mwilini mchana na usiku hata ukiwa kwenye feni kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali. Si lazima iwe homa au ugonjwa mmoja maalum.
Sababu zinazoweza kuchangia ni pamoa na;
- Homa au maambukizi: Hasa ikiwa una joto la mwili lililopanda, kutetemeka, uchovu au maumivu ya mwili.
- Mazingira yenye joto: Chumba chenye joto, mavazi mazito au mwili kutopata hewa ya kutosha.
- Msongo wa mawazo au wasiwasi: Unaweza kuongeza hisia ya joto na kusababisha kutokwa jasho.
- Tezi ya shingo kufanya kazi kupita kiasi: Inaweza kuambatana na mapigo ya moyo kwenda haraka, kutetemeka, kupungua uzito au kutokwa jasho sana.
- Mabadiliko ya homoni: Hali hii inaweza kutokea kutokana na mabadiliko mbalimbali ya homoni kulingana na umri na hali ya mtu.
- Baadhi ya dawa au vichocheo: Kafeini nyingi na baadhi ya dawa zinaweza kuongeza hisia ya joto au kutokwa jasho.
Nini cha kufanya?
Pima joto la mwili kwa kipimajoto wakati unahisi joto. Kuhisi mwili una joto pekee hakuthibitishi kuwa una homa.
Ikiwa hali hii inaendelea kwa siku kadhaa, inakusumbua wakati wa kulala au inaongezeka, ni vizuri kufanyiwa uchunguzi ili kutafuta chanzo.
Tafuta huduma ya afya mapema ikiwa joto linaambatana na homa, kutokwa jasho sana usiku, kupungua uzito bila sababu, mapigo ya moyo kwenda haraka, kikohozi cha muda mrefu au udhaifu mkubwa.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
22 Agosti 2026, 19:03:14

