top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

15 Oktoba 2026, 14:56:27

Mtoto kunyonya vidole nifanyaje aache?

Kunyonya vidole ni tabia ya kawaida kwa watoto, lakini ikiendelea kwa muda mrefu inaweza kuathiri mpangilio wa meno na ukuaji wa taya. Hapa kuna baadhi ya njia za kumsaidia mtoto kuacha tabia hii:


1. Mpe mambo mengine ya kufanya: Mpe mtoto michezo au shughuli za kumshughulisha ili kupunguza kunyonya vidole anapokuwa hana shughuli.

2. Mfariji kwa upole: Mtoto anapohitaji kujituliza, mkumbatie, mshike au msomee hadithi ili ajisikie salama.

3. Msifie anapojitahidi: Mpongeze anapokaa bila kunyonya vidole badala ya kumkaripia au kumwadhibu.

4. Zungumza naye: Mweleze kwa upole namna ya kuacha tabia hii na umsaidie kujifunza njia nyingine za kujituliza.

5. Epuka kumlazimisha: Usimfokee, kumwaibisha, kumwadhibu, kumfungia mikono au kupaka vitu vyenye ladha kali kwenye vidole ili kumzuia. Msaidie taratibu kwa uvumilivu, kwani kumlazimisha kunaweza kumletea hofu na msongo.

6. Tafuta ushauri wa Mtaalamu: Ikiwa tabia inaendelea baada ya miaka 3 au meno yanaanza kubadilika, zungumza na daktari wa meno.


Soma zaidi kuhusu makala hii kwa kubofya 👉Mtoto kunyonya Vidole.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

15 Oktoba 2026, 09:30:18

​

bottom of page