Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 10:31:25
Mtoto wangu anasumbuliwa na tonsils
Kuvimba kwa Tonsil(tonsilaitisi) kwa mtoto ikifahamika pia kama matezi kwa mtoto kunaweza kusababishwa na virusi au bakteria. Kwa watoto, maambukizi ya virusi ndiyo chanzo cha kawaida, hivyo si kila mtoto mwenye tonsil anahitaji antibiotiki.
Dalili zinazoweza kuonekana ni:
- Maumivu ya koo na kuumia wakati wa kumeza
- Tonsil kuvimba au kuwa nyekundu
- Homa
- Tezi limfu za shingo kuvimba
- Harufu mbaya mdomoni
- Madoa meupe au usaha kwenye tonsil
- Mtoto kukataa kula au kunywa kwa sababu ya maumivu
Ni muhimu mtoto achunguzwe ikiwa ana homa kubwa, usaha/madoa meupe kwenye tonsil, maumivu makali ya koo, au hali inajirudia mara kwa mara. Kipimo cha koo kinaweza kuhitajika kutofautisha maambukizi ya bakteria na virusi.
Mpeleke hospitali haraka ikiwa anapata shida kupumua, hawezi kumeza mate, anatokwa mate mengi, hawezi kunywa maji, sauti inabadilika sana, anaonekana dhaifu sana, au uvimbe wa koo unaongezeka.
Kwa mtoto mwenye tonsil zinazojirudia mara nyingi, daktari anaweza pia kutathmini kama kuna sababu ya kuhitaji matibabu maalum au kuondolewa kwa tonsil.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
2 Septemba 2026, 21:31:43

