Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
27 Septemba 2026, 15:44:17
Na je naweza tumia muda gani kukutana na mweza wangu baada ya mimba kuharibika?
Baada ya mimba kuharibika, muda wa kuanza kufanya tendo la ndoa hutegemea hali ya mwili na kama damu imeisha.
Kwa ujumla, ni vizuri kusubiri hadi kutokwa damu kuishe na maumivu ya tumbo yapungue au kuisha kabla ya kufanya tendo la ndoa. Hii husaidia kupunguza hatari ya maambukizi.
Ikiwa hakuna damu, maumivu, homa au uchafu wenye harufu mbaya, tendo la ndoa linaweza kuanza tena baada ya kupona.
Muhimu:
- Ujauzito mwingine unaweza kutokea haraka, hata kabla ya hedhi ya kwanza kurudi. Ikiwa hupangi kupata ujauzito, tumia njia za uzazi wa mpango.
- Ikiwa kuna damu nyingi, maumivu makali, homa, uchafu wenye harufu mbaya, kizunguzungu au kuzimia, usifanye tendo la ndoa na nenda hospitali kwa uchunguzi.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
23 Agosti 2026, 11:17:23

