Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 10:36:42
Na kwanini nikitumia kinga wakati wa tendo huwa zina chanika
Kinga (Kondomu) kuchanika mara kwa mara wakati wa tendo si jambo la kawaida. Mara nyingi husababishwa na matumizi, msuguano au aina ya kondomu.
Sababu zinazoweza kufanya kondomu ichanike ni:
- Kondomu kuwa ndogo sana au kutowiana vizuri na ukubwa wa uume.
- Ukavu ukeni, unaoongeza msuguano wakati wa tendo.
- Kutotumia vilainishi vya kutosha. Kama kondomu ni ya lateksi, epuka mafuta kama Vaseline, baby oil au mafuta ya kupikia kwa sababu yanaweza kuifanya lateksi idhoofike.
- Kuvaa kondomu vibaya, kwa mfano kutokubonyeza sehemu ya juu ili kuondoa hewa kabla ya kuivaa.
- Kutumia kondomu iliyopitwa na muda au iliyohifadhiwa sehemu yenye joto kali, kama kwenye gari au mfukoni kwa muda mrefu.
- Kufungua kifurushi kwa kucha, meno au kitu chenye ncha kali, na kuisababisha kuchanika kabla au wakati wa tendo.
- Kutumia kondomu mbili kwa wakati mmoja; msuguano kati yao unaweza kuongeza uwezekano wa kuchanika.
- Msuguano mkubwa kutokana na tendo kuwa kali au muda mrefu, hasa ikiwa hakuna lubricant ya kutosha.
Ikiwa kondomu inachanika mara kwa mara, jaribu ukubwa/aina nyingine ya kondomu, tumia lubricant inayolingana na aina ya kondomu, na hakikisha inawekwa vizuri kabla ya kuanza tendo.
Ikiwa kondomu imechanika wakati wa tendo na kuna uwezekano wa mimba au maambukizi ya zinaa, hatua za baada ya tendo zinaweza kuhitajika kulingana na muda uliopita na mazingira ya tendo.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
2 Septemba 2026, 18:29:26

