top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Natokwa na uchafu ukeni usio na harufu, shida itakuwa nini?

Uchafu wa ukeni usio na harufu mara nyingi unaweza kuwa ute wa kawaida wa uke, hasa ikiwa ni wa uwazi au mweupe, hauna muwasho, hauwashi na hauna maumivu. Kiasi na muonekano wa ute unaweza kubadilika kulingana na siku za mzunguko wa hedhi, hasa karibu na kipindi cha ovulation.


Hata hivyo, ikiwa uchafu umeongezeka au umebadilika na unaambatana na:

  • Muwasho au kuwaka ukeni: inaweza kuashiria fangasi au muwasho wa uke.
  • Uchafu mzito mweupe kama maziwa yaliyoganda: unaweza kuendana na fangasi.
  • Uchafu wa njano/kijani au maumivu wakati wa kukojoa: unaweza kuhitaji uchunguzi wa maambukizi, ikiwemo baadhi ya magonjwa ya zinaa.
  • Maumivu ya chini ya tumbo au maumivu wakati wa kufanya ngono: ni muhimu kupimwa ili kuondoa maambukizi ya uke au shingo ya kizazi.

Kama uchafu ni mweupe au uwazi, hauna harufu, hauna muwasho wala maumivu, mara nyingi hauhitaji dawa.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

9 Septemba 2026, 15:23:54

​

bottom of page