top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 17:41:41

Naumwa chembe ya moyo nifanyeje?

Maumivu ya chembe ya moyo (epigastriamu) ni maumivu sehemu ya juu katikati ya tumbo, chini kidogo ya kifua. Sababu zake zinaweza kuwa tofauti, hivyo tiba inategemea chanzo.


Sababu zinazoweza kuhusika ni:

  • Gastraitisi (kuvimba kwa ukuta wa tumbo)
  • Vidonda vya tumbo
  • Kucheua tindikali/kiungulia
  • Maambukizi ya H. pylori
  • Gesi tumboni au kutokula kwa muda mrefu
  • Baadhi ya dawa, hasa ibuprofen, diclofenac, aspirin na dawa nyingine za kundi la NSAIDs
  • Mara chache, maumivu kutoka kwenye nyongo, kongosho au moyo yanaweza kuhisiwa eneo hili.

Kwa maumivu ni mepesi bila dalili za hatari:

  • Kula milo midogo badala ya kula chakula kingi kwa mara moja.
  • Epuka pombe, sigara, kahawa nyingi na vyakula vinavyoongeza maumivu.
  • Epuka kutumia ibuprofen/diclofenac/aspirin bila ushauri wa mtaalamu ikiwa kuna uwezekano wa gastritis au kidonda cha tumbo.
  • Dawa za kupunguza acid zinaweza kusaidia ikiwa chanzo ni acid reflux/gastritis, lakini kama maumivu yanaendelea au kurudia, ni vizuri kupimwa.

Nenda hospitali haraka ikiwa maumivu ni makali sana au ya ghafla, yanaenea kifuani/mgongoni, yanaambatana na kupumua kwa shida, kutokwa jasho, kuzimia, kutapika damu, choo cheusi kama lami, au tumbo kuwa gumu sana.


Ikiwa maumivu yamerudia kwa siku kadhaa, yanatokea hasa baada ya kula au ukiwa na njaa, au yanaambatana na kichefuchefu/kiungulia, uchunguzi wa H. pylori na kidonda cha tumbo unaweza kuhitajika.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

27 Agosti 2026, 18:17:25

​

bottom of page