top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Naweza pata dawa ya kutokwa usaa kwenye sehemu ya siri?

Ndiyo, kutokwa usaha kwenye sehemu za siri kunaweza kutibiwa, lakini dawa inategemea chanzo cha maambukizi. Usaha unaweza kusababishwa na magonjwa ya zinaa kama gonorrhea au klamidia, au maambukizi mengine.


Kwa hiyo si salama kutumia antibayotiki yoyote bila kupima au kuchunguzwa, kwa sababu dawa na dozi hutofautiana kulingana na maambukizi.


Unachopaswa kufanya:

  • Nenda kituo cha afya upimwe gonorrhea na klamidia, na vipimo vingine vya Magonjwa ya zinaa kulingana na historia yako.
  • Kama kuna uwezekano wa Magonjwa ya zinaa, mwenza wa ngono naye anapaswa kupimwa na kutibiwa inapohitajika.
  • Epuka kufanya ngono bila kondomu hadi wewe na mwenza wako mtakapomaliza matibabu na kupewa ushauri wa daktari.
  • Usitumie antibayotiki iliyobaki nyumbani au dawa za kienyeji kwenye sehemu za siri.

Nenda hospitali haraka ikiwa usaha unaambatana na maumivu makali ya chini ya tumbo, homa, uvimbe wa korodani, au hali yako inazidi kuwa mbaya.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

4 Septemba 2026, 20:52:27

​

bottom of page