Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 14:27:13
Nilikuwa natamani kujua maji maji ya ukeni yanaambukiza UKIMWI ikiwa nina kidonda au ata ikigusa ngozi tu?
Maji maji ya ukeni yanaweza kuwa na VVU ikiwa mtu ana maambukizi ya VVU, lakini si kila mgusano wa maji hayo na ngozi husababisha maambukizi.
- Ikiwa maji ya ukeni yanagusa ngozi isiyo na mpasuko, isiyo na kidonda, kwa kawaida hayatoi njia ya kuambukiza VVU kwa sababu ngozi intact ni kinga nzuri.
- Ikiwa maji hayo yanaingia moja kwa moja kwenye kidonda wazi, jeraha linalotokwa damu, au kwenye utando wa ndani kama uke, sehemu ya ndani ya uume, njia ya haja kubwa au macho, kuna uwezekano wa maambukizi.
- Hatari pia hutegemea kiasi cha majimaji, aina ya exposure, na kama mtu mwenye VVU anatumia dawa na ana kiwango cha virusi kinachoonekana kwenye damu.
Muhimu: VVU haviambukizwi kwa kuguswa tu na ngozi ya kawaida. Pia haviambukizwi kupitia jasho, machozi au mate ya kawaida. Pia endapo kuna mipasuko midogo sana isiyoonekana kwa macho inaweza kuwa njia ya kupata maambukizi.
Ikiwa kulikuwa na mgusano wa maji ya ukeni na kidonda wazi ndani ya saa 72 zilizopita, ni muhimu kwenda kituo cha afya haraka kwa tathmini ya PEP, kwa sababu PEP hufanya kazi vizuri zaidi ikianza mapema.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
31 Agosti 2026, 13:33:38

