Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Nilitumia P2 baada ya kufanya ngono bila kinga, nikapata damu siku chache baadaye, lakini sasa hedhi yangu imechelewa. Je, inaweza kuwa ni kwa sababu ya P2 au ninaweza kuwa mjamzito?
P2 inaweza kubadilisha mzunguko wa hedhi. Baada ya kutumia dawa ya dharura, hedhi inaweza kuja mapema au kuchelewa, na unaweza pia kupata damu katikati ya mzunguko. Damu inayotokea baada ya kutumia P2 si lazima iwe hedhi yako ya kawaida.
Hata hivyo, kutokwa damu baada ya kutumia P2 hakuthibitishi kuwa hakuna ujauzito. P2 hupunguza uwezekano wa ujauzito lakini si kinga ya asilimia 100.
Kama hedhi yako imechelewa, fanya kipimo cha ujauzito. Ikiwa hujui kabisa siku ambayo hedhi ilipaswa kuanza, kipimo kinaaminika zaidi ukifanya angalau siku 21 baada ya tendo la mwisho la ngono bila kinga.
- Kama kipimo ni Hasi(huna mimba) lakini hedhi bado haiji, unaweza kurudia kipimo baada ya siku chache au kumuona mtoa huduma wa afya.
- Kama kipimo ni Chanya(una mimba), tafuta huduma ya afya kwa ajili ya tathmini zaidi.
- Kama una maumivu makali ya chini ya tumbo, hasa upande mmoja, kizunguzungu kikali, kuzimia, au kutokwa damu nyingi, nenda hospitali haraka.
Kwa hiyo, kuchelewa kwa hedhi baada ya P2 kunaweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni, lakini kipimo cha ujauzito ndicho kinachoweza kusaidia kujua kama kuna ujauzito.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
18 Septemba 2026, 05:34:20

