top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 14:00:44

Nimetumia cefixime capsule kama dawa ya gono lakini bado natokwa na usaha, nifanye nini?

Kwanza, ni muhimu kujua kwamba kutokwa na usaha/uchafu sehemu za siri hakumaanishi moja kwa moja kwamba ni gono au ni gono pekee. Dalili hizi zinaweza pia kusababishwa na maambukizi mengine ya njia ya mkojo au magonjwa mengine ya zinaa kama klamidia na maambukizi mengine ya yurethra.


Watu wengi huanza kutumia dawa wanayoamini ni ya gono bila kufanyiwa kipimo. Pia, kutumia dawa isiyofaa, dozi isiyofaa, kuacha dawa kabla ya muda uliopendekezwa au kupata maambukizi tena kutoka kwa mwenza ambaye hakutibiwa kunaweza kufanya dalili ziendelee.


Kwa hiyo, ikiwa kuna usaha unaendelea kutoka baada ya kutumia dawa:


  • Usiongeze au kurudia antibiotic mwenyewe bila uchunguzi.
  • Fanya kipimo cha gono, kama NAAT, na vipimo vingine vinavyofaa kulingana na dalili.
  • Daktari anaweza pia kuchunguza klamidiana sababu nyingine za yurethraitisi, kwa sababu si kila usaha unatokana na gono.
  • Ikiwa gono limethibitishwa na dalili zinaendelea baada ya matibabu sahihi, daktari anaweza kuhitaji kuchunguza uwezekano wa usugu wa dawa au maambukizi mapya. Katika hali inayoshukiwa kuwa kufeli kwa matibabu, kipimo cha kuotesha bakteria na kipimo cha usugu wa antibayotiki vinaweza kuhitajika.
  • Mwenza/wapenzi wa ngono pia wanahitaji kuchunguzwa na kutibiwa inapohitajika ili kuzuia maambukizi kurudi.

Kumbuka: Cefixime ni mojawapo ya dawa zinazoweza kutumika katika baadhi ya mazingira, lakini si dawa inayopendelewa kama tiba ya kwanza katika miongozo ya sasa; ceftriaxone ndiyo inayopendelewa katika miongozo ya Shirika la Afya Duniani. Cefixime pia imehusishwa na kupungua kwa uwezo wake w akutibu gono kutokana na usugu wa bakteria kwenye dawa hii.


Kwa hiyo, kwa mtu ambaye hajawahi kupimwa na amejinunulia cefixime kwa sababu tu anatokwa na usaha, hatua inayofaa si kubadilisha antibayotiki nyingine kiholela, bali kufanyiwa uchunguzi ili kujua chanzo cha usaha kwanza.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

25 Septemba 2026, 18:49:49

​

bottom of page