Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Nina tatizo la tumbo linauma kama lina kidonda. Tatizo linaweza kuwa nini?
Maumivu yanayohisiwa kama kuna kidonda tumboni, hasa sehemu ya juu ya tumbo, yanaweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au duodenum. Sababu kuu ni maambukizi ya bakteria H. pylori au matumizi ya dawa za maumivu aina ya NSAIDs kama ibuprofen, diclofenac na aspirin.
Sababu nyingine zinaweza kuwa:
- Gastraitisi: kuvimba kwa ukuta wa tumbo, kunaweza kusababisha maumivu, kuungua au kichefuchefu.
- Asidi nyingi tumboni/kurudisha tindikali: maumivu au hali ya kuungua inaweza kuongezeka baada ya kula au unapolala.
- Matatizo ya nyongo au kongosho: yanaweza kusababisha maumivu sehemu ya juu ya tumbo, wakati mwingine yakisambaa hadi mgongoni.
Kama maumivu yanaendelea, ni vizuri kupimwa hospitalini ili kubaini chanzo, hasa H. pylori ikiwa daktari ataona inahitajika. Usitumie dawa za maumivu kama ibuprofen au diclofenac bila ushauri, kwa sababu zinaweza kuongeza tatizo la tumbo.
Nenda hospitali haraka ikiwa unatapika damu, choo kinakuwa cheusi kama lami, una maumivu makali ghafla, unazimia au unakuwa dhaifu sana.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
11 Septemba 2026, 08:19:36

