Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Nina viupele kwenye kichwa cha uume, shida ni nini?
Vipele vidogo kwenye kichwa cha uume vinaweza kusababishwa na hali mbalimbali, na si kila kipele ni ugonjwa wa zinaa.
Sababu zinazowezekana ni:
- Vipele lulu (Pearly penile papules- PPP) – vipele vidogo, vya rangi ya ngozi au weupe, mara nyingi hupangwa kwa mstari kuzunguka ukingo wa kichwa cha uume. Si ugonjwa wa zinaa, si hatari na havihitaji matibabu.
- Sunzua sehemu za siri za uzazi (HPV) – vinaweza kuwa na muonekano wa vipele vilivyoinuka na wakati mwingine hukua au kuongezeka taratibu.
- Muwasho au mzio (demataitisi) kutokana na sabuni, mafuta, kondomu au bidhaa nyingine.
- Fangasi (Kandida) – mara nyingi huambatana na kuwasha, wekundu au ute.
- Folikulaitisi, ingawa huwa zaidi kwenye maeneo yenye vinyweleo kuliko kwenye kichwa chenyewe cha uume.
Muhimu: Muonekano pekee hauwezi kuthibitisha kama ni magonjwa ya zinaa. Usivipasue, kuvikamua au kupaka dawa bila kujua chanzo.
Kama vipele vinaongezeka, vinauma, vinatoa usaha, vinatoa damu, vinakuwa vidonda, au ulifanya ngono bila kinga hivi karibuni, ni vizuri kuonana na daktari wa ngozi/urology au kliniki ya magonjwa ya zinaa kwa uchunguzi.
Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
4 Septemba 2026, 18:35:55

