top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

27 Septemba 2026, 15:32:08

Ukiwa na mimba changa kufanya mapenzi mara kwa mara ni hatari?

Kwa ujauzito wa kawaida usio na matatizo, kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kwa ujumla si hatari kwa mimba changa.


Tendo la ndoa halisababishi mimba kuharibika katika ujauzito wa kawaida, na mtoto hulindwa ndani ya mfuko wa uzazi.


Hata hivyo, daktari anaweza kushauri kuacha au kupunguza tendo la ndoa ikiwa kuna:

  • Kutokwa damu ukeni, hasa ikiwa kuna maumivu.
  • Maumivu makali ya tumbo au nyonga.
  • Tatizo la mlango wa kizazi au placenta linalohitaji tahadhari.
  • Historia au dalili zinazoashiria hatari ya mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati.
  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Baada ya tendo, baadhi ya wajawazito wanaweza kupata maumivu madogo ya tumbo au damu kidogo, lakini damu nyingi, maumivu makali, kizunguzungu/kuzimia au maumivu ya upande mmoja wa tumbo vinahitaji uchunguzi wa haraka.


Kwa hiyo, mara ngapi mnafanya tendo si jambo kuu, muhimu ni hali ya ujauzito na kama kuna sababu yoyote ya kitabibu inayohitaji kuepuka tendo la ndoa.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

23 Agosti 2026, 11:22:43

​

bottom of page