top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

10 Oktoba 2026, 08:40:14

Unaweza kupata mimba ukiwa na kijiti cha uzazi wa mpango?

Inawezekana kupata mimba ukiwa na kijiti cha uzazi wa mpango, lakini ni nadra sana ikiwa kijiti kimewekwa vizuri na kinatumika ndani ya muda wake wa ufanisi.


Kijiti cha uzazi wa mpango ni miongoni mwa njia zenye ufanisi mkubwa wa kuzuia mimba, lakini hakuna njia ya uzazi wa mpango yenye ufanisi wa 100%.


Mimba inaweza kutokea ikiwa:


  • Kijiti cha uzazi wa mpango hakikuwekwa vizuri au hakikuwekwa kabisa.
  • Kimekaa muda mrefu kuliko muda uliopendekezwa na mtengenezaji au mhudumu wa afya.
  • Kijiti kiliwekwa wakati tayari kulikuwa na ujauzito.
  • Kuna matumizi ya baadhi ya dawa zinazoweza kupunguza ufanisi wa kijiti cha uzazi wa mpango, kwa mfano baadhi ya dawa za kifafa, rifampicin/rifabutin na baadhi ya dawa za HIV.
  • Kwa nadra sana, mimba inaweza kutokea licha ya kijiti cha uzazi wa mpango kufanya kazi vizuri.

Ikiwa kuna dalili za ujauzito ukiwa na kijiti cha uzazi wa mpango, ni vizuri kufanya kipimo cha ujauzito. Ikiwa kipimo ni chanya, nenda kituo cha afya kwa uchunguzi, kwa sababu ujauzito unaotokea wakati wa kutumia implant unahitaji kutathminiwa na mtaalamu.


Kumbuka: Kutokwa damu kidogo, kutokwa damu bila mpangilio au kukosa hedhi wakati wa kutumia implant ni jambo linaloweza kutokea na peke yake hakumaanishi kuwa kuna mimba.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

4 Septemba 2026, 01:00:20

​

bottom of page