top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 12:57:45

Upungufu wa madini chuma unaweza kusababisha upungufu wa damu?

Mwili unapokosa chuma cha kutosha, hutengeneza hemoglobini kidogo. Hali hii huitwa Upungufu wa damu wa madini chuma.


Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Uchovu na udhaifu
  • Kizunguzungu au maumivu ya kichwa
  • Kupumua kwa shida hasa wakati wa shughuli
  • Moyo kwenda mbio
  • Ngozi kuwa nyeupe/pale kuliko kawaida
  • Kucha kuwa dhaifu au kuvunjika kirahisi
  • Kutamani kula vitu visivyo chakula, kama udongo au barafu (pica), kwa baadhi ya watu

Muhimu: Si kila upungufu wa damu unasababishwa na upungufu wa madini chuma. Kuna sababu nyingine kama upungufu wa vitamin B12/folate, magonjwa sugu, kupoteza damu, malaria na magonjwa ya kurithi kama seli mundu au thalassemia.


Kipimo cha CBC/FBC pamoja na feritini kinaweza kusaidia kuonyesha kama upungufu wa damu unatokana na upungufu wa chuma.


Pata zawadi kwa kutoa maoni yako kuboresha mfumo huu, Bofya 👉Shiriki.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

1 Septemba 2026, 14:11:08

​

bottom of page