top of page

Uzazi wa mpango

Kipandikizi chini ya ngozi, njiti ya uzazi wa mpango, kijiti cha uzazi wa mpango

Njiti (kijiti) ya uzazi wa mpango

Njiti ya uzazi wa mpango ni njia salama, ya muda mrefu na yenye ufanisi mkubwa inayowekwa chini ya ngozi ili kuzuia mimba kwa miaka kadhaa. Hufanya kazi kwa kutoa homoni ya projesteroni pekee, kinafaa hata kwa mama anayenyonyesha, na uwezo wa kushika mimba huweza kurudi haraka baada ya kuondolewa.

kidonge cha p2

P2: Vidonge vya dharura vya uzazi wa mpango

P2 yenye levonorgestrel hufanya kazi vizuri zaidi ikitumiwa mapema, ndani ya saa 72 baada ya tendo lisilo na kinga, na inaweza kusababisha mabadiliko ya muda katika homoni na mzunguko wa hedhi. Kutumia mara kwa mara hakusababishi utasa wala mabadiliko ya kudumu ya homoni, lakini haitoi kinga dhidi ya mimba kwa tendo linalofuata wala dhidi ya maambukizi ya zinaa.

Sindano ya uzazi wa mpango

Sindano ya uzazi wa mpango

Huwa na kemikali medroxyprogesterone acetate inayofanya kazi kama kichocheo cha progesterone kuzuia ujauzito kwa muda wa wiki 14 ingawa sindano huchomwa kila baada ya miezi mitatu kukamilika.

Upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi

Upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi

Uzazi wa mpango wa kudumu ni njia salama na yenye ufanisi wa zaidi ya 99% kwa watu waliokamilisha mpango wao wa kupata watoto. Ni uamuzi wa maisha unaohitaji kufanywa kwa umakini mkubwa kwani haukusudiwi kurekebishwa baadaye.

Vidonge vya uzazi wa mpango wa dharura, dawa za kuzuia mimba iiingie

Uzazi wa Mpango wa Dharura: Mwongozo Kamili

Uzazi wa mpango wa dharura ni njia salama ya kuzuia mimba baada ya kufanya ngono bila kinga, endapo utatumika mapema ndani ya muda unaopendekezwa. Husaidia kuzuia mimba isitunge lakini haupaswi kutumika kama mbadala wa uzazi wa mpango wa kudumu.

bottom of page