top of page

Vidokezo vya Afya

Kipindi cha tatu cha ujauzito

Kipindi cha tatu cha ujauzito

Huanzia wiki ya 28 hadi 40 ya ujauzito na huwa kipindi cha mwisho cha safari ya ujauzito. Kijusi hukua kutoka urefu wa sentimita 23 kufikia 48 hadi 53 na kuongezeka uzito kutoka gramu 820 hadi kilo 2 hadi 4.

Kiungo usichokitumia kwa muda mrefu hudhoofika

Kiungo usichokitumia kwa muda mrefu hudhoofika

Kuna ukweli wa kisayansi kutoka kwenye tafiti kuthibitisha usemi wa 'Kiungo cha mwili kisichotumika kwa muda mrefu, hudhoofika na kutofanya kazi yake vema'. Hivyo hivyo mwanaume asiyeshiriki ngono kwa muda mrefu, homoni testosterone inayompa nguvu za kiume na hamu ya mapenzi hupungua kwenye damu kulingana na siku asizoshiriki ngono.

Kiwango cha Hb kinachoamua kuongezwa damu

Kiwango cha Hb kinachoamua kuongezwa damu

Uamuzi wa kuongezwa damu hutegemea hali ya afya na dalili zinazoonekana kutokana na upungufu wa damu. Kiwango chini ya 5g/dl kikiambatana au kutoambatana na dalili hulazimu mtu aongezewa damu.

Klamidiasisi huonekana baada ya muda gani?

Klamidiasisi huonekana baada ya muda gani?

Kutokwa na ute mweupe kwenye uume au uke unaoambatana na maumivu wakati wa kukojoa au hedhi katikati ya vipindi ni miongoni mwa dalili zinazoonekana siku ya 7 hadi 28 tangu kushiriki ngono zembe.

Kucheua kwa watoto

Kucheua kwa watoto

Kucheua kwa watoto ni hali ya kawaida inayotokea muda mfupi baada ya kunyonya. Hata hivyo wakati mwingine huashiria tatizo kubwa hususani ikiambatana na dalili nyingine kama kutokuongezeka uzito n.k.

bottom of page