top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, M.D

Mhariri:

Dkt. Helen R, M.D

Jumatano, 19 Julai 2023

Kiwango cha Hb kinachoamua kuongezwa damu

Kiwango cha Hb kinachoamua kuongezwa damu

Kuongezwa damu ni mchakato unaohusisha kuongeza mazao ya damu kwenye mzunguko wa damu wa mtu mwingine. Uongezaji wa damu hutegemea tatizo lililopo na hulenga kurejesha kiwango kilichopotea na kinachotakiwa ili masha kuendelea.


Kuna miongozo mbalimbali ya kidunia imewekwa kwa ajili ya kuelekeza ni kiwango cha damu ambacho huhesabiwa kama himoglobini (Hb) kinafaa kurejeshwa kawaida kwa kuongezwa damu. Mara nyingi hata hivyo uamuzi wa kuongezwa damu hutegemea hali ya afya na dalili zinazoonekana kutokana na upungufu wa damu. Makala hii imeelezea kuhusu kiwango cha chini cha Hb cha kuongezwa damu na madhara ya kuongezwa damu.

 

Miongoza ya chama cha Benki ya damu ya Amerika,  inashauri kudhibiti ongezo la damu kwa wagonjwa wasio na dalili yoyote licha ya kuwa na kiwango cha damu chini ya 13g/dl kwa wanaume au 12g/dl kwa wanawake ikiwa upungufu wa damu hautokani na kuvuja kwa damu. Licha ya kutumika kwa udhibiti huo sasa, mwongozo wa zamani uliweka kiwango cha chini cha kuongeza damu bila kujali dalili kuwa 10g/dl.


Nchi nyingi duniani zina viwango vyake vya udhibiti pia, ikihusisha kiwango cha chini kuwa 7g/dl bila kuwa na dalili zozote , wakati zingine zimeweka kiwango cha chini kuwa 5g/dl bila kuwa na dalili.


Tafiti zinashauri wagonjwa wanaotarajia kufanyiwa upasuaji wa mifupa au wenye ugonjwa wa mishipa ya ateri ya koronari waongezewe damu kama wana HB chini ya 8g/dl

 

Mwongozo wa wagonjwa mahututi inashauri kiwango cha chini cha kuongezwa damu kuwa 7g/dl. Kuongezwa damu kunaweza kuamuliwa kwa wagonjwa wenye hali ya kuvuja damu au kuvia damu, wagonjwa wenye dalili za upungufu wa damu ( kama mapigo ya moyo kwenda kasi, kuishiwa pumzi, uchovu mkali) na kuwa na kiwango cha damu chini ya 8g/dl. Upungufu wa damu kwa wagonjwa hawa hutokana na upungufu wa kiwango cha hemoglobini inayozunguka mwilini kwenye damu. Upungufu huo unaweza kutoka kutokana na sababu za nje ya mwili, uzalishaji duni, uharibifu ndani ya mwili au muunganiko wa sababu mbalimbali.


Wakati wagonjwa wanaotokwa na damu hupata upungufu wa damu, upunfugu huo kama wenyewe hauwezi kuwa sababu ya kuongezwa damu.


Chama cha madaktari wa usingizi kianshauri mgonjwa kuongezwa damu anapokuwa na kiwango cha himoglobini cha 6g/dl au pungufu.

 

Viashiria vya kuongezwa damu

Viashiria vya kuongezwa damu ni sababu, hali au magonjwa yanayopelekea mtu kuongezwa damu, viashiria hivyo vimelezwa katika aya zilizopita na kuorodheshwa hapa chini pia;


 • Kuvuja damu sambamba na kuwa na dalili za upungufu wa damu wakati kiwango cha damu ni chini ya 8g/dl

 • Kuwa na kiwango cha damu cha 6g/dl au pungufu hali unatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mifupa au kuwa na ugonjwa wa moyo

 • Kubadilisha damu

 • Kiwango cha damu chini ya 8g/dl kwa mgonjwa wa moyo

 • Kuwa na damu chini ya 8g/dl kwa mgonjwa anayetakiwa kufanyiwa upasuaji

 • Mgonjwa anayetakiwa kupata matibabu ya mionzi na ana damu chini ya 10g/dl

 • Mgonjwa anayetakiwa kupata matibabu ya dawa za saratani na ana damu chini ya 9g/dl kabla na baada ya matibabu

 • Kuwa na damu 5g/dl pamoja na au pasipo kuwa na dalili za upungufu wa damu

 • Kuwa mahututi mwenye kiwango cha damu 7g/dl au pungufu

 • Kuongezea plazma ya damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo, wenye ini kuferi kwa hatua za mwisho, na ugonjwa mkali wa kusambaa wa kuganda damu mwilini, kuongezwa damu zaidi ya 10g/dl ndani ya masaa 24

 • Kuongezwa plazma ya damu kwa wagonjwa waliozidishiwa dozi ya warfarini na hatari ya kuvuja damu ama kuwa na ugonjwa wa kuvuja damu unaohatarisha Maisha

 • Kuwa na upungufu wa chembe sahani za damu zinazosaidia damu kuganda 

 • Kuwa na upungufu wa fibrinojeni na hatari ya kutoka damu, kupata jeraha, kufanyiwa upasuaji mkubwa, au  kuwa na ugonjwa mkali wa kusambaa wa kuganda damu mwilini.


Kiwango gani cha damu kinapaswa kuongezwa kwa mara moja?

Isipokuwa kama mgonjwa anavuja damu, inashauriwa kuongezwa chupa moja kwa wakati mmoja na chupa nyingine baada ya kipimo cha wingi wad amu kufanyika baada ya kuongezwa chupa ya awali. Chupa moja ya damu huongeza hemoglobini 1 na  asilimia 3 ya kiwango cha chembe nyekundu za damu.


Mwongozo wa kuongeza damu kwa Tanzania

Mwongozo wa matibabu wa mwaka 2021 unatoa maelekezo ya kuongezwa damu sawa na maelezo yaliyoelezewa katika aya iliyopita.


Maudhi na Madhara ya kuongezwa damu

Kuna madhara mbalimbali ya kuongezwa damu ambayo wataalamu wa afya huyazingatia kabla na baada ya kuongezwa damu ili kupunguza uwezeko wa kuyapata ambayo ni;

 • Maambukizi kama ya kirusi cha homa ya ini B,C, UKIMWI n.k

 • Mwitikio wa kufisha wa uharibifu wa chembe nyekundu za damu ambao ni kwa nadra sana

 • Mzio wa damu

 • Majeraha kwenye mapafu

 • Kuzidi kwa kiwango cha damu

 • Kuharibika kwa usawia wa madini kwenye damu

 

Je umepima na kukutwa na upungufu wa damu?

Kufahamu kama unapaswa kuongezwa damu au la wasiliana na daktari wako au daktari wa ULY CLINIC.


Wapi unapata maelezo zaidi?

Soma makala zifuatazo kwa maelezo zaidi kuhusu


Makala hii pia imeeleza kuhusu

 • Wagonjwa wapi wanapaswa kuongezwa damu?

 • Hali zipi husababisha mtu kuongezwa damu?

 • Sababu zipi za kuongezewa damu

 • Madhara ya kuongezewa damu

 • Maudhi ya kuongezewa damu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 15:29:53

Rejea za mada hii:

1. Sturgis CC. THE HISTORY OF BLOOD TRANSFUSION. Bull Med Libr Assoc. 1942 Jan;30(2):105-12. [PMC free article] [PubMed]

2. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK499824/#article-18403.r1. Imechukuliwa 18.07.2023

3. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK499824/#. Imechukuliwa 18.07.2023

4. Tanzania Standard treatment guideline @2021

5. What is a blood transfusion? National Heart, Lung, and Blood Institute. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/bt. Imechukuliwa 18.07.2023

6. The process. American Red Cross. http://www.redcrossblood.org/learn-about-blood/blood-transfusions/the-process. Imechukuliwa 18.07.2023

7. Getting a blood transfusion. American Cancer Society. https://www.cancer.org/treatment/treatments-and-side-effects/treatment-types/blood-transfusion-and-donation/how-blood-transfusions-are-done.html. Imechukuliwa 18.07.2023

8. Blood safety basics. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/bloodsafety/basics.html. Imechukuliwa 18.07.2023

bottom of page