top of page

Vidokezo vya Afya

Majira yenye vichocheo viwili na saratani

Majira yenye vichocheo viwili na saratani

Matumizi ya majira yenye vichocheo viwili licha ya kupunguza hatari ya kupata saratani ya ovari na kizazi, huongeza hatari ya kupata saratani ya matiti kwa zaidi ya asilimia 20 na shingo ya kizazi kwa kiasi kidogo.

Mama anayenyonyesha anaweza kutoa maziwa anapofika kileleni

Mama anayenyonyesha anaweza kutoa maziwa anapofika kileleni

Mama anayenyonyesha anaweza kutokwa na maziwa anapofika kileleni, mwitikio huu hutegemea mida ya kufanya ngono, uzoefu wa mama kunyonyesha na umri wa mtoto. Endapo kutoa maziwa ni kero kwa mpenzi wako, wakati wa ngono funga matiti yako kwa nguo nzuri inayoweza kufyonza maziwa yanayotoka

Mama mjamzito mwenye kisukari

Mama mjamzito mwenye kisukari

Mama mjamzito mwenye ugonjwa wa kisukari toa taarifa juu ya ugonjwa wako ili umkinge mwanao na kushuka kwa sukari mwilini.

Manjano kwa mtoto

Manjano kwa mtoto

Manjano kwa mtoto ni dalili ya hatari kwani inaweza kupelekea matatizo ya ubongo. Muwahishe mtoto hospitali pindi uonapo dalili hii kwa tiba.

Mara ngapi utumie dawa ya minyoo?

Mara ngapi utumie dawa ya minyoo?

Watoto wenye umri wa miezi 12 au zaidi na watu wazima wanaoishi mikoa yenye hali ya juu ya maambukizi ya minyoo wanashauriwa kunywa albendazole au mebendazole kama kinga mara moja hadi mbili katika mwaka.

bottom of page