top of page

Vidokezo vya Afya

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline

Muda sahihi kusoma kipimo cha HIV SD bioline

HIV 1/2 SD BIOLINE 3.0 ni kipimo cha haraka chenye uwezo wa kutambua uwepo wa antibodi zilizozalishwa na mfumo wa kinga ya mwili kupambana na maambukizi ya kirusi HIV1 au HIV2. Majibu ya kipimo ni sahihi kama yatasomwa ndani ya dakika 10 hadi 20, majibu baada ya muda huu si ya kuaminika.

Muda unaotosha kulala

Muda unaotosha kulala

Muda wa kulala kiafya hutegemea umri wa mtu na hupungua kwa jinsi umri unavyoongezeka. Mfano kichanga anapaswa kulala angalau muda wa masaa 14 hadi 17, vijana wadogo, masaa 7 hadi 9, wazee wa miaka 65 na zaidi, ni masaa 7 hadi 8 wakati wa usiku. Lala muda wa kutosha kwa afya yako

Muda wa kusubiri ngono baada ya kutoa mimba

Muda wa kusubiri ngono baada ya kutoa mimba

Unaweza kushiriki ngono muda wowote ikiwa unahisi mwili upo tayari na damu nyingi imeacha kutoka ukeni. Kutumia kinga na kuchelewa kidogo huzuia hatari ya maambukizi kwenye kizazi na mimba nyingine.

Namna ya kufanya mtoto ale na kukua vema

Namna ya kufanya mtoto ale na kukua vema

Ili mtoto ale na kukua vema, muandalie chakula kutoka kwenye makundi mbalimbali, kula pamoja naye, usimlazimishe kula endapo ameshiba au hana njaa, mpe maji ya kunywa katika kiwango kinachoshauriwa kwa siku, usimpe vinywaji vya sukari, kama soda, mbadala wake mpatie maziwa mgando au juisi halisi, mpe milo midogo ya kiafya katikati ya milo mikuu mitatu ya siku, baadhi ya nyakati usihofu mtoto anapokataa kulana Kuwa mfano wa kuigwa kwa kula mlo kamili.

Ngono baada ya kujifungua

Ngono baada ya kujifungua

Wenza wanatakiwa kuwa na mzungumzo ya wazi kuhusu ngono a kufahamu mabadiliko ya mama baaada ya kujifungua ili kuwa na mahusiano mazuri katika kipindi hiki cha mpito

bottom of page