top of page

Vidokezo vya Afya

Ukweli kuhusu mzunguko wa hedhi wa siku 28

Ukweli kuhusu mzunguko wa hedhi wa siku 28

Zaidi ya wanawake 65 kati ya 100 hawapati mzunguko wa hedhi wa siku 28. Kama mzunguko wako unabadilika kila mwezi na upo ndani ya siku 21 hadi 32, usihofu wala kutafuta tiba kwa kuwa ni wa kawaida.

Umri mzuri wa kushika mimba

Umri mzuri wa kushika mimba

Mwanamke anapozaliwa huwa na mayai takribani milioni 2 yanayopungua kadri umri unavyoongezeka. Mayai elfu 25 husalia kwenye umri wa miaka 37 na elfu 1 kwenye umri wa miaka 51. Ili kushika ujauzito wenye matokeo mazuri kwako na mtoto, shika baada ya miaka 20 na kabla ya miaka 35.

Umuhimu wa FEFO

Umuhimu wa FEFO

FEFO huzuia na kutibu upungufu wa damu unaosababishwa na upungufu wa madini chuma na vitamin B9.

Umuhimu wa maziwa ya mama

Umuhimu wa maziwa ya mama

Pamoj na matibabu atakayo patiwa mtoto mchanga anayeumwa maziwa ya mama ni muhimu. Mnyonyeshe mwanao mara kwa mara kujenga afya yake.

Unapima mara ngapi VVU baada ya kuanza PEP?

Unapima mara ngapi VVU baada ya kuanza PEP?

Kipimo cha VVU hurudiwa baada ya miezi 3 na 6, hakuna haja ya kurudia baada ya muda huu isipokuwa endapo kuna kihatarishi endelevu au una ujauzito.

bottom of page