top of page
Vidokezo vya Afya

Watoto ni wasambazaji wakubwa wa COVID-19
Tafiti mpya zinaonyesha kuwa watoto wa umri wa miaka 0 hadi 22 ni wasambazaji wakubwa wa virusi vinavyosababisha COVID-19 licha ya kutoonyesha dalili zozote zile kama ilivyo kwa watu wazima. ULY CLINIC inakushauri uzingatie tahadhari za kujikinga na maambukizi kama kuvaa barakoa, kunawa mikono, kuepuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

Zuia kusafirisha vimelea vya maradhi unapokohoa
Magonjwa mengi ya mfumo wa hewa kama Kifua kikuu, mafua ya virusi, nimonia na mengine husafirishwa kwa njia ya matone ya maji maji yanayotoka wakati mtu anakohoa au kupiga chafya. Zuia magonjwa haya kwa kufunika kinywa chako na kitambaa, tishu au kiwiko cha mkono.
bottom of page


