top of page
Vidokezo vya Afya

Hedhi baada ya uzazi wa mpango
Baada ya kuacha matumizi ya njia za uzazi wa mpango zenye vichochezi, hedhi yako inapaswa kurejea ndani ya siku 90, hata hivyo inaweza chukua kipindi kati ya wiki 18 hadi 22 kama unatumia sindano ya depo-provera. Wasiliana na daktari mzunguko wako wa hedhi usiporejea kwenye hali ya kawaida siku 90 baada ya kuacha kutumia vichochezi vya uzazi wa mpango.

Hisia za chuchu huongezeka kipindi cha kunyonyesha
Chuchu za mama anayenyonyesha huwa na hisia kali zinaponyonywa na mtoto, hata hivyo, njia hii huwa haifanyi kazi ya kuamsha hisia kali za kingono endapo ikitumika na mpenzi. Kuamsha ngono kwa kuchezea chuchu haitakiwi kuwa uchaguzi wa kwanza kwa wanawake wanaonyonyesha.
bottom of page



