Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je, maziwa ya mama yanaweza kuwa na Virusi vya UKIMWI (VVU)?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Endelea na ARV kila siku na kupima kiwango cha virusi. Nyonyesha maziwa pekee miezi 6, kisha ongeza vyakula. Mtoto apate dawa ya kinga na vipimo vya VVU kliniki ya CTC/RCH. Soma Kunyonyesha kama uzazi wa mpango.
Maelezo
Kinachoongeza hatari
Mama hatumii ARV au virusi vingi.
Maambukizi mapya ya mama wakati wa kunyonyesha.
Kuchanganya vyakula na maziwa ya mama kabla ya miezi 6.
Chuchu kuchubuka, titi kuvimba (mastitis), vidonda mdomoni kwa mtoto.
Kinga
ARV kwa mama kila siku; kiwango cha virusi kupimwa wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Mtoto – dawa za kinga (mfano nevirapine, na zidovudine kwa walio hatarini zaidi) kwa wiki 6–12.
Vipimo vya mtoto – wiki 6, na baadaye kwa ratiba, na baada ya kuacha kunyonya.
Mama asiye na VVU – apime tena wakati wa kunyonyesha; atumie kondomu au PrEP kama mwenza ana hatari.
Nini cha kufanya
Usiache ARV hata siku moja.
Tibu chuchu zilizochubuka na maumivu ya titi mapema.
Lishe bora kwa mama – soma Vyakula vya kuongeza maziwa.
Maziwa ya kopo – tu kama yanapatikana salama, kwa maji safi, na kwa uamuzi na mtoa huduma.
Dalili za hatari
Mtoto homa, kuharisha au kushindwa kunyonya – hospitali.
Titi jekundu, kuvimba na homa – kituoni mapema.
Lini umwone daktari
Umesahau ARV mara kadhaa.
Kiwango cha virusi hakijapimwa.
Unapanga kuacha kunyonyesha – mtoto apimwe.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Maziwa ya mama yana VVU?
Ndiyo kwa mama mwenye VVU; ARV hupunguza hatari sana.
2. Mama mwenye VVU anyonyeshe?
Ndiyo, akiwa kwenye ARV, kwa ushauri wa kliniki.
3. Hatari ni kiasi gani kwa ARV?
Chini ya 1% virusi visipopimika.
4. Kwa nini maziwa pekee miezi 6?
Kuchanganya huongeza hatari ya maambukizi.
5. Mtoto apewe dawa?
Ndiyo, dawa za kinga kwa wiki 6–12.
6. Mtoto apimwe lini?
Wiki 6 na kwa ratiba ya kliniki.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:07:17
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Guideline: updates on HIV and infant feeding. Geneva: WHO; 2016.
World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV prevention, testing, treatment, service delivery and monitoring. Geneva: WHO; 2021.
Flynn PM, et al. Prevention of HIV-1 transmission through breastfeeding: efficacy and safety of maternal antiretroviral therapy versus infant nevirapine prophylaxis (PROMISE). J Acquir Immune Defic Syndr. 2018;77(4):383–92.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

