top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je, ni salama kutumia PEP mara kwa mara?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: PEP inaweza kurudiwa kwa kila tukio la hatari halisi. Kufua nguo hakuambukizi VVU. Ukihitaji PEP mara nyingi – uliza kuhusu PrEP. Soma Mambo ya kuzingatia kwenye PEP.



Maelezo


Matukio yanayohitaji PEP


  • Ngono bila kondomu au kondomu kupasuka na mtu mwenye VVU au asiyejulikana hali yake.

  • Kuchomwa sindano yenye damu.

  • Damu kuingia kwenye jeraha wazi, macho au mdomo.


Yasiyohitaji PEP


  • Kufua nguo, kushikana mikono, kuchangia vyombo.

  • Jasho, mate, machozi – soma Majimaji gani yana VVU.

  • Damu iliyokauka muda mrefu kwenye ngozi isiyo na jeraha.


PEP ya pili


  • Huanzishwa upya kwa tukio jipya, baada ya kipimo cha VVU.

  • Tukio jipya ukiwa bado kwenye PEP – kwa kawaida endelea; mtoa huduma ataamua kuongeza siku 28 kuanzia tukio jipya.

  • Maudhi hufanana na mara ya kwanza – kichefuchefu, kichwa, uchovu.


Nini cha kufanya



Dalili za hatari


Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:


  • Tukio jipya la hatari ndani ya saa 72 – soma Dawa za kuzuia UKIMWI.

  • Upele mkubwa, macho kuwa njano ukiwa kwenye PEP.


Lini umwone daktari


  • Umetumia PEP zaidi ya mara moja mwaka huu.

  • Hujapimwa VVU wiki 12 baada ya tukio la mwisho.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Naweza kutumia PEP mara ya pili?

Ndiyo, kwa tukio jipya la hatari, ndani ya saa 72.

2. Kufua nguo za mtu mwenye VVU kunaambukiza?

Hapana; PEP haihitajiki.

3. PEP mara nyingi ina madhara?

Dawa za sasa ni salama kwa siku 28; madhara ni maudhi madogo.

4. Tukio jipya nikiwa kwenye PEP?

Endelea na dawa; mtoa huduma ataamua kuongeza siku.

5. PrEP ni nini?

Dawa za kila siku za kuzuia VVU kwa walio katika hatari mara kwa mara.

6. Nipime lini?

Kabla ya kila PEP na wiki 12 baada ya tukio la mwisho.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:08:28

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Guidelines for HIV post-exposure prophylaxis. Geneva: WHO; 2024.

  2. Tanner MR, et al. Antiretroviral postexposure prophylaxis after sexual, injection drug use, or other nonoccupational exposure to HIV – CDC recommendations, United States, 2025. MMWR Recomm Rep. 2025;74(1).

  3. World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV prevention, testing, treatment, service delivery and monitoring. Geneva: WHO; 2021.

bottom of page