top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Je, ukiwa na maambukizi ya VVU (HIV) kichwa huuma vipi?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Kichwa kuuma si kipimo cha VVU – pima. Mwenye VVU mwenye kichwa kikali kinachoendelea, homa, kutapika au kuona ukungu – hospitali leo. Soma Dalili za VVU ndani ya kichwa.


Maelezo


Maambukizi mapya


  • Kichwa, homa, koo kuuma, vipele, tezi – wiki 2–4.

  • Hupotea ndani ya wiki 1–2.

  • Pima – soma Kipimo cha VVU.


Wanaoishi na VVU


  • Visababishi vya kawaida – msongo, kipandauso, sinus, macho.

  • ARV – kichwa kidogo wiki za mwanzo kwa baadhi.

  • Kinga ndogo – cryptococcus, TB, toxoplasmosis; soma Meningitis.


Vipimo vya kichwa kikali


  • CD4, CrAg ya damu.

  • Maji ya uti wa mgongo.

  • CT/MRI.


Nini cha kufanya


  • ARV kila siku.

  • Maji, usingizi, kupunguza kahawa.

  • Paracetamol kwa kichwa kidogo.

  • Mweleze mtoa huduma kichwa kipya baada ya kuanza ARV.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kichwa kikali pamoja na homa, shingo kukakamaa, kutapika.

  • Kuona ukungu, kuchanganyikiwa, degedege.

  • Udhaifu wa upande mmoja.


Lini umwone daktari


  • Kichwa kinachoendelea zaidi ya wiki 1.

  • Kichwa kipya baada ya kubadilisha ARV.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Kichwa kuuma ni dalili ya VVU?

Si peke yake; pima.

2. Kichwa cha VVU kinatofautiana?

Hakuna sifa maalum.

3. ARV husababisha kichwa?

Kwa baadhi, kwa muda mfupi.

4. Kichwa kikali kwa mwenye VVU?

Huweza kuwa cryptococcus au TB – hospitali.

5. Kila mwenye VVU hupata kichwa?

Hapana.

6. CrAg ni nini?

Kipimo cha damu cha cryptococcus.

Imeandikwa:

2 Julai 2026, 12:08:01

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Guidelines for diagnosing, preventing and managing cryptococcal disease among adults, adolescents and children living with HIV. Geneva: WHO; 2022.

  2. World Health Organization. Consolidated guidelines on HIV prevention, testing, treatment, service delivery and monitoring. Geneva: WHO; 2021.

  3. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page